Revision 1003434 of "Professor Jay" on swwiki{{Msanii muziki 2
|Jina = Professor Jay
|Background = solo_singer
|Img =
|Img capt =
|Jina la kuzaliwa = Joseph Haule
|P.a.k = Jay Wamitulinga, Heavy wait MC, Daddy
|Asili yake = [[Dar es Salaam]], [[Tanzania]]
|Amezaliwa = {{birth date|1975|12|29|df=yes}}
|Aina = [[Muziki wa hip hop|Hip hop]]
|Kazi yake = Mbunge (jimbo la Mikumi - Mkoani Morogoro), [[Kurap|Rapper]], [[mtunzi wa nyimbo]],
|Miaka ya kazi =
|Studio =
|Ameshirikiana na = [[Lady Jay Dee]], [[Juma Nature]], [[Inspector Haroun]], [[Black Rhino]], [[Simple X]], [[Q Chillah]], [[A.Y.]], [[Mangwair]]
|Tovuti = http://www.Professorjay.net
}}
'''Joseph Haule''' (amezaliwa [[tarehe]] [[29 Desemba]] [[1975]]) ni [[Mtanzania]] [[msanii]] wa [[muziki wa hip hop]] na vilevile [[mwanasiasa]] wa [[Chama cha kisiasa]] cha [[Chama cha Demokrasia na Maendeleo]] (CHADEMA). Amechaguliwa kuwa [[Wabunge wa Tanzania 2015|mbunge]] wa [[Mikumi]] kwa miaka [[2015]] – [[2020]]. <ref>[http://www.parliament.go.tz/administrations/262 Tovuti ya Bunge la Tanzania], iliangaliwa Mei 2017</ref>
Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii '''Professor Jay'''. Katika Tanzania anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee wasikilize [[muziki]] wa [[Bongo Flava]]. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la [[Hard Blasters Crew]] - [[Chemsha Bongo]]. Kundi hilo ni moja ya makundi yaliyofanya muziki hup, ambao hujulikana kama 'muziki wa kizazi kipya', kukubaliwa na sehemu kubwa ya Watanzania.
== Maisha ya muziki ==
Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo [[miaka ya 1990]] na alijiunga na kundi la '[[Hard Blasters Crew]]' (HBC) mwaka [[1994]]. Mwaka [[1995]] Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini [[Tanzania]].
Jay na HBC walitoa [[albamu]] ya kwanza iitwayo 'Funaga Kazi' mwaka [[2000]]. Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini [[Tanzania]]. Albamu hii yenye [[ujumbe]] mzito ina nyimbo kama 'Chemsha Bongo' na 'Mamsapu' ambazo zilichangia kufanya muziki wa 'Bongo Flava' kuwa wa kila [[rika]] na kupewa [[heshima]]. Kabla ya hapo muziki huo ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni.
== Msanii binafsi ==
Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo [[2001]] na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo "Machozi Jasho na Damu". Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya apate [[tuzo]] ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa wimbo wake wa 'Ndio Mzee' kutoka kwenye albamu hiyo, wkifuatiwa na wimbo wa "Piga Makofi na Bongo [[Dar es Salaam]]"
[[Mwaka]] [[2003]] alitoa albamu ya pili iitwayo "Mapinduzi Halisi" ambayo nayo ilishinda tuzo ya [[Kili Music Awards]] kuwa albamu bora ya muziki wa Hip Hop nchini [[Tanzania]] kwa [[mwaka]] [[2003]]. Albamu hii imebeba nyimbo kama "Zali la Mentali", "Msinitenge," na "Promota Anabeep"
[[Mwaka]] [[2006]] [[Januari]] alitoa albamu ya tatu iliyoitwa "J.O.S.E.P.H". Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka [[Mwanzo]] kabla ya albamu kutoka. Wimbo huu ulichaguliwa kuwa wimbo bora wa [[Bongo Flava]] kwenye [[BBC]] na [[Radio One Awards]].
Mpya imewahi kuteuliwa kuwa albamu bora ya Hip Hop, [[mtunzi]] bora wa nyimbo za Hip Hop, na [[Nyimbo]] bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. [[2006]]."Nikusaidieje" na baadaye [[Kisima Music Awards]] ya [[Kenya]] ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini [[Tanzania]].
== Tuzo Alizopata ==
* '''1''' [[Kili Music Awards]] ([[2003]])
* '''2''' [[BBC]], [[Radio One Awards]] ([[2006]])
* '''3''' [[Kili Music Awards]] ([[2006]])
== Muhtasari wa Albamu ==
* '''1''' Aluta Continua ([[2007]]) Ipo Njiani [[Kutolewa]]
* '''2''' J.O.S.E.P.H. ([[2006]])
* '''3''' [[Mapinduzi]] Halisi ([[2003]])
* '''4''' [[Machozi]] [[Jasho]] na [[Damu]] ([[2001]])
== Alioshirikiana nao kimuziki ==
* '''1''' [[Lady Jay Dee]]. ( [[Bongo]] [[Dar es Salaam]] na Nimeamini)
* '''2''' [[Mc Babu Ayubu]]. ( Ndio Mzee )
* '''3''' [[Juma Nature]]. ( Ndio Mzee na Zali la Mentali )
* '''4''' [[Q Chilah]]. ( Msinitenge )
* '''5''' [[Inspector Haroun]]. ( Hakuna Noma )
* '''6''' [[Simple X]]. ( Piga Makofi na Hakuna Noma )
* '''7''' [[Jose Chameleone]]. ( Ndivyo Sivyo - Kutoka [[Uganda]] )
* '''8''' [[Adil a.k.a Hisabati]]. ( Tunawakilisha na Rapper Msaidizi kwenye Ziara - Kutoka [[Tanzania]] )
==Tanbihi==
{{reflist}}
==Viungo vya nje==
[http://www.Professorjay.net Professor Jay Tovuti Binafsi]
[http://www.kwetubongo.com Kwetu Bongo]
<p>[http://www.swahiliremix.com Tovuti ya Swahili Remix]</p>
{{Mbegu-wanasiasa-Tanzania}}
[[Jamii:Waliozaliwa 1975]]
[[Jamii:Watu walio hai]]
[[Jamii:Wanasiasa wa Tanzania]]
[[Jamii:Bunge la Tanzania]]
[[Jamii:Wanamuziki wa Tanzania]]All content in the above text box is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike license Version 4 and was originally sourced from https://sw.wikipedia.org/w/index.php?oldid=1003434.
![]() ![]() This site is not affiliated with or endorsed in any way by the Wikimedia Foundation or any of its affiliates. In fact, we fucking despise them.
|