Revision 1194131 of "Unafiki" on swwiki'''Unafiki''' ni utovu wa [[ukweli]] katika mwenendo wa [[binadamu]] hasa kwa lengo la kujipatia sifa, k. mf. kama mwanadini [[maadili|mwadilifu]].
Tofauti na [[mkosefu]], mnafiki anatenda vema kwa nje, lakini nia yake si kufuata [[dhamiri]] yake na maadili anayojua ni mazuri, bali ni kupendeza watu wengine ili kupata faida fulani kutoka kwao.
Ni jambo linalolaumiwa sana katika [[dini]] zote, hasa [[Ukristo]], kutokana na lawama za [[Yesu]] dhidi ya viongozi wengi wa [[Uyahudi]]. [[Injili]] zinasisitiza hasa lawama zake dhidi ya baadhi ya [[Mafarisayo]].
NB: mtu anaweza kukosa kitu anachokiitaji kutoka kwa mungu sababu ya unafiki. [[esùbe-mwenebatu-justin]]
{{mbegu-elimu}}
[[Jamii:Maadili]]
[[Jamii:Saikolojia]]All content in the above text box is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike license Version 4 and was originally sourced from https://sw.wikipedia.org/w/index.php?oldid=1194131.
![]() ![]() This site is not affiliated with or endorsed in any way by the Wikimedia Foundation or any of its affiliates. In fact, we fucking despise them.
|