Revision 776071 of "Mkoa wa Magharibi" on swwiki

{{mergefrom|Mkoa wa Magharibi (Kenya)|date=July 2010}} 
[[File:Kenya-Western.png|thumb|right|175px|Eneo la Mkoa wa Magharibi nchini Kenya.]]
[[File:Kenya-relief-map-towns.jpg|thumb|300px| Mji mkuu wa Mkoa wa Magharibi wa Kenya ni Kakamega (click to enlarge map)]]
[[File:Kenya westp.jpg|frame|Wilaya nne za jadi za mkoa wa Magharibi, Kenya.]]
'''Mkoa wa Magharibi'''  nchini [[Kenya]], unaopakana na [[Uganda]], ni mojawapo ya mikoa ya utawala ya [[Kenya]] nje ya [[Nairobi]]. Uko magharibi mwa [[Bonde la Ufa]] la [[Mashariki]] na ni makao kwa watu asili ya [[Waluhya]]. [[Maadili ya Quakers]] ni maarufu sana hapa. Mlima wa pili kwa urefu nchini Kenya, [[Mlima Elgon]] uko katika [[Wilaya ya Bungoma]]. [[Msitu wa Kakamega]] ni sehemu ya eneo hili. Makao makuu yake ni mji wa [[Kakamega]]. Mwaka wa 1999 idadi ya jumla ya wakazi ilikuwa 3,358,776 katika eneo la 8,361 km ².

== Jiografia ==
Mkoa wa Magharibi una maumbile mbalimbali ya mazingira, kuanzia vilima vya kaskazini mwa Bungoma hadi eneo tambarare linalopakana na [[Ziwa Victoria]] katika [[Wilaya ya Busia]]. Eneo la juu zaidi katika Mkoa wa Magharibi ni kilele cha [[Mlima Elgon]], la chini zaidi ni mji wa [[Busia]] kwenye maji ya [[Ziwa Victoria]].

== Hali ya hewa ==
Hali ya hewa ni ya [[kitropiki]], ikiwa na tofauti kutokana na kimo. Wilaya ya Kakamega huwa na joto na unyevu karibu mwaka mzima, ilhali wilaya ya Bungoma ni baridi kidogo lakini ina unyevu uo huo. Wilaya ya Busia ndio yenye joto zaidi, ilhali Wilaya ya Vihiga yenye vilima ndio baridi zaidi. Eneo zima hupata mvua kubwa mwaka wote, na mvua za masika katika miezi ya kwanza ya mwaka.

== Uchumi ==
Kilimo ndiyo shughuli kuu ya kiuchumi katika mkoa huu.

Wilaya ya Bungoma ni eneo la sukari, ikiwa na mojawapo ya viwanda vya sukari kubwa nchini, pamoja na viwanda vidogovidogo kwa kusaga sukari. [[Mahindi]] pia yanalimwa kwa kujikimu kinyumbani, pamoja na [[mtama]] na [[mawele]]. Kilimo cha maziwa hufanyika sana, na vilevile ufugaji wa kuku. Kuna mtaji mdogo lakini muhimu wa kitalii, unaoegemea sherehe za tohara zinazofanyika kila baada ya miaka miwili.

Wilaya ya Kakamega ina mchanganyiko wa kilimo cha kujikimu na mazao ya fedha, huku ukuzaji wa [[miwa]] ukiwa kifua mbele mbele ya mazao mengine yanayokuzwa. Wilaya hii ina viwanda viwili vya sukari. Pia kuna mtaji muhimu wa utalii unaoegemea [[Msitu wa Kakamega]].

Wilaya ya Busia hupokea mvua za mafuriko kutoka [[mto Nzoia]], na shughuli ya kiuchumi iliyopewa kipa mbele ni uvuvi katika [[Ziwa Victoria]]. Kilimo cha kibiashara kiasi pia hufanyika, hasa miwa. Ukulima wa kujikimu wa [[mihogo]] umeenea sana.

Wilaya ya Vihiga ina mashamba makubwa ya [[chai]], na ndio eneo la mashambani lenye watu wengi zaidi nchini Kenya. Uchimbaji mawe kwa ajili ya vifaa vya ujenzi ni shughuli muhimu katika wilaya hii yenye milima. Kilimo cha maziwa mojawapo ya shughuli zinazofanyika sana Vihiga.

Magharibi Kenya ina viwanda vingi vikubwa, vikiwemo vya sukari (viwanda 4). Kubwa zaidi kati ya hivi ni kile cha [[Mumias]], chenye makao yake mjini Mumias, magharibi mwa Kakamega. Kiwanda hiki ndicho kinachotoa aina ya sukari maarufu zaidi nchini Kenya na ni mfano wa mafanikio ya kiuchumi. Pia katika Magharibi Kenya kuna kiwanda kikubwa zaidi cha karatasi Afrika (Pan Paper Mills kilichoko [[Webuye)]] na pamoja na viwanda vya kutengenezea kemikali. Hata hivyo, hali ya maisha kwa ujumla iko chini na huduma za kijamii kama maji ya bomba na umeme hazipatikani kwa wengi wa wakazi wa eneo hili.

== Wilaya ==
''Wilaya''  {{smaller|(''capital'')}}<br>
[[Bungoma]] {{smaller|(''[[Bungoma]]'')}} {{·}} 
[[Busia]] {{smaller|(''[[Busia, Kenya|Busia]]'')}} {{·}} 
[[Butere / Mumias]] {{smaller|(''[[Butere]]'')}} {{·}} 
[[Kakamega]] {{smaller|(''[[Kakamega]]'')}} {{·}} 
[[Lugari]] {{smaller|(''[[Lugari]]'')}} {{·}} 
[[Mlima Elgon]] {{smaller|(''[[Kapsokwony]]'')}} {{·}} 
[[Teso]] {{smaller|(''[[Malaba town|Malaba]]'')}} {{·}} 
[[Vihiga]] {{smaller|(''[[Vihiga]]'')}}

=== Wilaya baada ya 2007 ===

Wilaya Kadhaa mpya ziliundwa mwaka wa 2007 nchini Kenya, pia katika eneo la Magharibi <ref>[16] ^ [http://www.provincialadministration.go.ke/detail.php?op=8008 Ministry of State for Provincial Administration and National Security]</ref>

{| class="wikitable"
! Wilaya 
! Makao makuu
|-
|  [[Bungoma Mashariki]] (Webuye) 
|  [[Webuye]]
|-
|  [[Bungoma Kaskazini]] 
|  [[Kimilili]]
|-
|  [[Bungoma Kusini]] 
|  [[Bungoma]]
|-
|  [[Bungoma Magharibi]] (Sirisia) 
|  [[Chwele]]
|-
|  [[Bunyala]] 
|  [[Budalangi]]
|-
|  [[Busia]] 
|  [[Busia]]
|-
|  [[Kisumu Butere]] 
|  [[Butere]]
|-
|  [[Emuhaya]] 
|  [[Kima]]
|-
|  [[Hamisi]] 
|  [[Hamisi]]
|-
|  [[Kakamega Kaskazini]] (Malava) 
|  [[Malava]]
|-
|  [[Kakamega Kusini]] 
|  [[Kakamega]]
|-
|  [[Lugari]] 
|  [[Lumakanda]]
|-
|  [[Mlima Elgon]] 
|  [[Kapsokwony]]
|-
|  [[Mumias]] 
|  [[Mumias]]
|-
|  [[Samia]] 
|  [[Funyala]]
|-
|  [[Vihiga]] 
|  [[Mbale]]
|}

==Marejeo==
{{Reflist}}
{{Refimprove|date=November 2006}}

{{First and second-level administrative divisions of Kenya}}

{{coord|0|30|N|34|35|E|region:KE_type:adm1st_source:GNS-enwiki|display=title}}

==Marejeo==
{{Reflist}}

[[Jamii:Mkoa wa Magharibi (Kenya)]]
[[Jamii:Mikoa ya Kenya]]

[[ro:Provincia Western, Kenya]]