Revision 875943 of "Lava" on swwiki

'''Lava''' ni mwamba katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa [[dunia]] mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "[[magma]]" badala ya lava. 

Lava inatoka nje kwa kawaida penye [[volkeno]] wakati wa mlipuko. Ikipoa inakuwa [[mwamba]] imara.

Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600[[°C]] hadi 1200 °C. Katika hali hii inasambaa nje ya shimo la [[kasoko]]. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.


<gallery>
Image:Stromboli Eruption.jpg|Mlipuko wa volkeno ya [[Stromboli]] ([[Italia]])- kile chekundu kwenye picha ni lava.
Image:Aa_large.jpg|Mto wa lava kwenye volkeno ya [[Kilauea]] ([[Hawaii]])
Image:PahoehoeLava.jpg|Lava ikipoa inaweza kuonekana hivyo. 
Image:Nyiragongo lava lake.jpg|Ziwa la lava ndani ya [[kasoko]] ya mlima [[Nyiragongo]] huko [[Goma]] (Kongo)
Image:Kalapana_house_destroyed_by_lava.jpg|Mto wa lava inavyoharibu nyumba huko Hawaii mwaka 1990
</gallery>

[[Jamii:Volkeno]]
[[Jamii:Jiolojia]]

[[jv:Lava]]