Revision 880043 of "Elgon (mlima)" on swwiki

{{mergefrom|Mlima Elgon}}
[[Image:Mount elgon topo.jpg|thumb|250px|Eneo la Mlima Elgon]]
'''Mlima Elgon''' ni [[volkeno]] inayolala mpakani wa [[Uganda]] na [[Kenya]]. [[Kasoko]] yake ina kipenyo cha [[kilomita]] nane. 

Elgon ni mlima mkubwa wa pili nchini Kenya baada ya [[Mlima Kenya]]. Upande wa Uganda ni mlima mkubwa wa mashariki ya nchi lakini milima ya [[safu ya Ruwenzori]] ni kubwa kushinda Elgon.
 
Jina la mlima limetokana na [[Waelgonyi]] walioishi upande wa kusini wa mlima. [[Wamaasai]] hutumia jina "Ol Doinyo Ilgoon" na upande wa Uganda huitwa "Masawa".

Kuna vilele vitano:
* ''Wagagai''  (4,321 m), upande wa Uganda
* ''Sudek''    (4,302 m), upande wa Kenya
* ''Koitobos'' (4,222 m), upande wa Kenya
* ''Mubiyi''   (4,211 m), upande wa Kenya
* ''Masaba''   (4,161 m), upande wa Kenya

Mito ya [[Suam (mto)|Suam]], [[Nzoia (mto)|Nzoia]] na [[Turkwel (mto)|Turkwell]] ina chanzo kwa mlima huu. 
Vilele vya mlima ni sehemu ya hifadhi ya taifa pande zote mbili za Uganda na Kenya.

Miji ya karibu ni [[Kitale]], [[Bungoma]] na [[Webuye]] upande wa Kenya, halafu [[Tororo]] na [[Mbale]] upande wa Uganda.

{{Mbegu-jio-Uganda}}

[[Jamii:Milima ya Uganda|Elgon]]
[[Jamii:Milima ya Kenya|Elgon]]
[[Jamii:Volkeno za Afrika]]