Revision 889023 of "Amani (mwanamuziki)" on swwiki'''Cecilia Wairimu''' (alizaliwa mnamo 1980 mjini [[Thika]]), anafahamika zaidi kwa jina lake la jukwaa '''Aman''' i, ni mwanamuziki wa pop kutoka [[Kenya]]. Ameshinda tuzo mbalimbali, ikiwemo tuzo la mwanamke mwanamuziki bora katika tuzo za MAMA (MTV Africa Music Awards) mwaka wa 2009.
== Wasifu ==
Alisomea katika shule ya Upili ya Bishop Gatimu Ngandu, ambako alikuwa katika kundi la accapella la ''Sobriety'' . Amani saini mkataba wa [[Ogopa Deejays]] mwaka wa 1999, punde tu alipomaliza skuli ya upili. Nyimbo yake ya kwanza "Move on" ilienea sana katika stesheni za redio na ilifuatwa na nyimbo zingine kama vile "Tahidi" na "Papii".
Ushirikiano wake na [[Nameless]] mwaka wa 2002 katika nyimbo, 'Ninanoki', pia ilienea sana Nyimbo zake za baadaye zinajumuisha "Talk to You" (ikiwashirikisha Patonee na Big Pin), "Bad Boy" (ikimshirikisha Nyashinski wa [[Kleptomaniax]]), Usiwe Mbali (ikimshirikisha [[AY]]), "Tamani", "Missing My Baby" na "Tonight"
Albamu yake ya kwanza, ''Amani'' ilitolewa mwaka wa 2006 na kufuatiwa na ''Tamani'' . Ametembelea nchi ya [[Marekani]] na nchi nyinginezo
== Tuzo / Kuchaguliwa ==
=== Tuzo ===
* Tuzo za muziki ya Kisima mwaka wa 2006 - sanii mwanadada wa mwaka <ref name="kisimaawards.co.ke">6] ^ Kisima Awards winners 2007</ref>
* Tuzo za muziki ya Kisima mwaka wa 2006 - ushirikiano wa mwaka( "Bad Boy" na Nyashiski) <ref name="kisimaawards.co.ke" />
* 2006 Tuzo za CHAT - Msanii maarufu mwanadada <ref name="few">[8] ^ The Standard, Pulse Magazine, 5 Mei 2006: [http://www.eastandard.net/archives/cl/mags/pulse/articles.php?articleid=1143952035&date=5/5/2006 wateule wachache]</ref>
* 2006 Tuzo za CHAT - nyimbo maarufu <ref name="few" />
* 2006 Tuzo za CHAT - Ushirikiano maarufu <ref name="few" />
* Tuzo za muziki ya Kisima 2007 - mwandada boomba <ref>6] ^ Washindi wa Kisima Awards 2007</ref>
* 2007 Tuzo za muziki za lulu la Afrika (tuzo za PAM) - Msanii bora (Kenya) <ref>Museke: [http://www.museke.com/node/1617 Pearl of Africa Music (PAM) Awards 2007 Washindi - Uganda]</ref>
* 2009 MTV Africa Music Awards - Msanii bora mwandada <ref>Museke: [http://lyrics.fienipa.com/en/node/4273 MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2009 winners]</ref>
=== Kuchaguliwa ===
* 2002 Tuzo za CHAT <ref name="few" />
* 2006 Tuzo za muziki za lulu la Afrika - Msanii mwanadada bora wa Kenya<ref>Musicuganda.com: [http://www.musicuganda.com/pamnominees2006.html PAM 2006 nominees]</ref>
* Tuzo za muziki za Tanzania 2007 - Nyimbo bora katika Afrika ta Mashariki ( "Bad Boy") <ref>[http://www.kilitimetz.com/awards/2007/nominees_2007.html Tanzania Music Awards - 2007 Nominees]</ref>
* Tuzo za muziki za Tanzania 2007 - Nyimbo bora katika Afrika ta Mashariki ( "Missingmy Baby") <ref>[http://kilitimetz.com/awards/2008/nominees_2007.php Tanzania Music Awards - 2008 Nominees]</ref>
* 2008 Tuzo za video za muziki za Channel - video bora ya R & B barani Afrika( "Missing My Baby") <ref name="mio">Music Industry Online: [http://www.mio.co.za/newsitem.php?id=3185 2008 Tuzo za video za muziki za Channel O Nominees]</ref>
* 2008 Tuzo za video za muziki za Channel O - Nyimbo bora ya Afrika Mashiriki ( "Missing My Baby") <ref name="mio" />
* 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Nyimbo bora ya mwanadada ( "Tonight") <ref name="n3780">Museke: [http://museke.com/en/node/3780 2009 Channel O Africa Music Video Awards nominees]</ref>
* 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Video bora ya R & B video( "Tonight") <ref name="n3780"/>
* 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Bora Afrika Mashariki ( "Tonight") <ref name="n3780"/>
* 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Video ya mwaka( "Tonight") <ref name="n3780"/>
== Marejeo ==
{{Marejeo}}
[[Jamii:Waliozaliwa 1980]]
[[Jamii:Waliohai]]
[[Jamii:Wanamuziki wa Kenya]]All content in the above text box is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike license Version 4 and was originally sourced from https://sw.wikipedia.org/w/index.php?oldid=889023.
![]() ![]() This site is not affiliated with or endorsed in any way by the Wikimedia Foundation or any of its affiliates. In fact, we fucking despise them.
|