Revision 976926 of "Zaha" on swwiki'''Zaha''' (pia: '''lava'''; [[ing.]] [[w:lava|lava]]) ni mwamba katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa [[dunia]] mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "[[magma]]" badala ya zaha. Zaha inatoka nje kwa kawaida penye [[volkeno]] wakati wa mlipuko. Ikipoa inakuwa [[mwamba]] imara. Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600[[°C]] hadi 1200 °C. Katika hali hii inasambaa nje ya shimo la [[kasoko]]. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba. <gallery> Image:Stromboli Eruption.jpg|Mlipuko wa volkeno ya [[Stromboli]] ([[Italia]])- kile chekundu kwenye picha ni zaha. Image:Aa_large.jpg|Mto wa zaha kwenye volkeno ya [[Kilauea]] ([[Hawaii]]) Image:PahoehoeLava.jpg|Zaha ikipoa inaweza kuonekana hivyo. Image:Nyiragongo lava lake.jpg|Ziwa la zaha ndani ya [[kasoko]] ya mlima [[Nyiragongo]] huko [[Goma]] (Kongo) Image:Kalapana_house_destroyed_by_lava.jpg|Mto wa zaha inavyoharibu nyumba huko Hawaii mwaka 1990 </gallery> [[Jamii:Volkeno]] [[Jamii:Jiolojia]] All content in the above text box is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike license Version 4 and was originally sourced from https://sw.wikipedia.org/w/index.php?oldid=976926.
![]() ![]() This site is not affiliated with or endorsed in any way by the Wikimedia Foundation or any of its affiliates. In fact, we fucking despise them.
|