Revision 976930 of "Zaha" on swwiki

<sup>Kwa kutaja watoto wa wadudu angalia makala ya [[lava]]</sup>
[[File:Lava Lake Nyiragongo 2.jpg|thumb|right|300px|Ziwa ya lava kwenye [[Mlima Nyiragongo]] katika [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]]]]
'''Zaha''' (pia: '''lava'''; [[ing.]] [[w:lava|lava]]) ni [[mwamba (jiolojia)|mwamba]] ulio katika hali ya [[kiowevu]] kutokana na joto kali. Chini ya uso wa [[dunia]] mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "[[magma]]" badala ya zaha. Sawa na magma yenyewe zaha inaweza kuwa nzito kama uji-uji au nyepesi kama maji-maji. <ref name=camilla>{{cite book | last = | first = | authorlink = | coauthors = | title = Earth Science| publisher = Holt, Rinehart and Winston, Austin, Texas| date = 2001| pages = | url = | doi = | id = | isbn = 0-03-055667-8}}</ref> .

Zaha inatoka nje kwa kawaida penye [[volkeno]] wakati wa mlipuko. Inaweza kutoka pia katika ufa kwenye ganda la dunia.

Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600[[°C]] hadi 1200&nbsp;°C. Ndani ya shimo la [[kasoko]] ya [[volkeno]] lava inaweza kukaa kama ziwa la kuchemka. 

Ikitoka nje ya kasoko inaweza kuwa kama mto wa moto. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.

Ikipoa inaganda na kuwa [[mwamba (jiolojia)|mwamba]] imara

<gallery>
Image:Stromboli Eruption.jpg|Mlipuko wa volkeno ya [[Stromboli]] ([[Italia]])- kile chekundu kwenye picha ni zaha.
Image:Aa_large.jpg|Mto wa zaha kwenye volkeno ya [[Kilauea]] ([[Hawaii]])
Image:PahoehoeLava.jpg|Zaha ikipoa inaweza kuonekana hivyo. 
Image:Nyiragongo lava lake.jpg|Ziwa la zaha ndani ya [[kasoko]] ya mlima [[Nyiragongo]] huko [[Goma]] (Kongo)
Image:Kalapana_house_destroyed_by_lava.jpg|Mto wa zaha inavyoharibu nyumba huko Hawaii mwaka 1990
</gallery>

== Marejeo ==
<references/>


[[Jamii:Volkeno]]
[[Jamii:Jiolojia]]