Revision 983411 of "Professor Jay" on swwiki

{{Msanii muziki 2
|Jina = Professor Jay
|Background = solo_singer
|Img =
|Img capt =
|Jina la kuzaliwa = Joseph Haule
|P.a.k = Jay Wamitulinga, Heavy wait MC, Daddy
|Asili yake = [[Dar es Salaam]], [[Tanzania]]
|Amezaliwa = {{birth date|1975|12|29|df=yes}}
|Aina = [[Muziki wa hip hop|Hip hop]]
|Kazi yake = Mbunge (jimbo la Mikumi - Mkoani Morogoro), [[Kurap|Rapper]], [[mtunzi wa nyimbo]],
|Miaka ya kazi =
|Studio =
|Ameshirikiana na = [[Lady Jay Dee]], [[Juma Nature]], [[Inspector Haroun]], [[Black Rhino]], [[Simple X]], [[Q Chillah]], [[A.Y.]], [[Mangwair]]
|Tovuti = http://www.Professorjay.net
}}
'''Joseph Haule''' (amezaliwa tar. [[29 Desemba]] [[1975]]) ni msanii wa [[muziki wa hip hop]] ambaye vilevile ni Mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo la Mikumi kutoka mkoa wa Morogoro nchini [[Tanzania]]. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama '''Professor Jay'''. Katika Tanzania, Prof. Jay anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee waweze kusikiliza muziki wa Bongo Flava. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la Hard Blasters Crew - [[Chemsha Bongo]]. Professor Jay anatokea kundi la [[Hard Blasters Crew]]. Kundi hili ni moja ya makundi yaliyofanya muziki huu ambao hujulikana kama 'muziki wa kizazi kipya' kukubaliwa na sehemu kubwa ya wa [[Tanzania]].

== Maisha ya muziki ==
Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 90 hivi na alijiunga na kundi la '[[Hard Blasters Crew]]'(HBC) mnamo mwaka [[1994]]. Mwaka [[1995]] Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini [[Tanzania]]. Jay na HBC walitoa albamu ya kwanza iitwayo 'Funaga Kazi' mwaka [[2000]] Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini [[Tanzania]]. Albamu hii yenye ujumbe mzito ina nyimbo kama  'Chemsha Bongo' na 'Mamsapu' ambazo zilichangia kufanya muziki wa '[[Bongo Flava]]' kuwa wa kila rika na kupewa heshima. Kabla ya hapo muziki huu ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni.

== Msanii Binafsi ==
Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo [[2001]] na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo "Machozi Jasho na Damu". Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya Prof. Jay kupata tuzo ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa nyimbo yake ya 'Ndio Mzee' kutoka kwenye albamu hiyo. na ikifuatiwa na Nyimbo ya "Piga Makofi na  Bongo [[Dar es Salaam]]"

[[Mwaka]] [[2003]] Alitoa albamu ya pili iitwayo "Mapinduzi Halisi" ambayo nayo ilishinda tuzo ya [[Kili Music Awards]] kuwa albamu bora ya [[Muziki]] wa Hip Hop nchini [[Tanzania]] kwa [[mwaka]] [[2003]]. Albamu hii imebebanNyimbo kama "Zali la Mentali", "Msinitenge," na "Promota Anabeep"

[[Mwaka]] [[2006]] [[Januari]] alitoa albamu ya tatu iliyoitwa "J.O.S.EP.P.H".  Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka [[Mwanzo]] kabla ya Albamu kutoka. Nyimbo hii ilichaguliwa kuwa nyimbo bora ya [[Bongo Flava]] kwenye [[BBC]] na [[Radio One Awards]].

Mpya imewahi [[kuteuliwa]] kuwa ni albamu bora ya Hip Hop , [[Mtunzi]] bora wa nyimbo za Hip Hop, na [[Nyimbo]] bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. [[2006]]."Nikusaidieje". na Baadae
[[Kisima Music Awards]] ya [[Kenya]] ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini [[Tanzania]].

== Tuzo Alizopata ==
* '''1''' [[Kili Music Awards]] ( [[2003]] )
* ''' 2''' [[BBC]], [[Radio One Awards]] ( [[2006]] )
* '''3''' [[Kili Music Awards]] ( [[2006]] )

== Muhtasari wa Albamu ==
* '''1''' Aluta Continua  ( [[2007]] ) Ipo Njiani [[Kutolewa]]
* '''2''' J.O.S.E.P.H.    ( [[2006]] )
* '''3''' [[Mapinduzi]] Halisi ( [[2003]] )
* '''4''' [[Machozi]] [[Jash]]o na [[Damu]] ( [[2001]] )

== Alioshirikiana nao kimuziki ==
* '''1''' [[Lady Jay Dee]]. ( [[Bongo]] [[Dar es Salaam]] na Nimeamini)
* '''2''' [[Mc Babu Ayubu]].   ( Ndio Mzee )
* '''3''' [[Juma Nature]].  ( Ndio Mzee na Zali la Mentali )
* '''4''' [[Q Chilah]].     ( Msinitenge )
* '''5''' [[Inspector Haroun]]. ( Hakuna Noma )
* '''6''' [[Simple X]].          ( Piga Makofi na Hakuna Noma )
* '''7''' [[Jose Chameleone]].    ( Ndivyo Sivyo - Kutoka [[Uganda]] )
* '''8''' [[Adil a.k.a Hisabati]].    ( Tunawakilisha na Rapper Msaidizi kwenye Ziara - Kutoka [[Tanzania]] )

==Viungo vya Nje==
[http://www.Professorjay.net Professor Jay Tovuti Binafsi]
[http://www.kwetubongo.com Kwetu Bongo]
<p>[http://www.swahiliremix.com Tovuti ya Swahili Remix]</p>

{{DEFAULTSORT:Professor Jay}}
[[Jamii:Waimbaji wa Tanzania]]
[[Jamii:Hip Hop ya Bongo]]
[[Jamii:Bongo Flava]]
[[Jamii:Muziki wa Kizazi Kipya]]
[[Jamii:Waliozaliwa 1975]]
[[Jamii:Watu walio hai]]