Difference between revisions 1016974 and 1016975 on swwiki

{{Msanii muziki 2
|Jina = Professor Jay
|Background = solo_singer
|Img =
|Img capt =
|Jina la kuzaliwa = Joseph Haule
|P.a.k = Jay Wamitulinga, Heavy wait MC, Daddy
|Asili yake = [[Dar es SalaamSongea]], [[Tanzania]]
|Amezaliwa = {{birth date|1975|12|29|df=yes}}
|Aina = [[Muziki wa hip hop|Hip hop]]
|Kazi yake = Mbunge (jimbo la Mikumi - Mkoani Morogoro), [[Kurap|Rapper]], [[mtunzi wa nyimbo]],
|Miaka ya kazi =Miaka ya 1990-hadi sasa
|Studio =
|Ameshirikiana na = [[Lady Jay Dee]], [[Juma Nature]], [[Inspector Haroun]], [[Black Rhino]], [[Simple X]], [[Q Chillah]], [[A.Y.]], [[Mangwair]], [[Taff B.]]
|Tovuti = http://www.Professorjay.net
}}
'''Joseph Haule''' (amezaliwa [[tarehe]] [[29 Desemba]] [[1975]]) ni [[Mtanzania]] [[msanii]] wa [[muziki wa hip hop]] na vilevile [[mwanasiasa]] wa [[Chama cha kisiasa]] cha [[Chama cha Demokrasia na Maendeleo]] (CHADEMA). Amechaguliwa kuwa [[Wabunge wa Tanzania 2015|mbunge]] wa [[Mikumi]] kwa miaka [[2015]] – [[2020]]. <ref>[http://www.parliament.go.tz/administrations/262 Tovuti ya Bunge la Tanzania], iliangaliwa Mei 2017</ref>  

Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii '''Professor Jay''' (zamani '''Nigga Jay'''). Katika Tanzania anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee wasikilize [[muziki]] wa [[Bongo Flava]]. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la [[Hard Blasters Crew]] - [[Chemsha Bongo]]. Kundi hilo ni moja ya makundi yaliyofanya muziki hup, ambao hujulikana kama 'muziki wa kizazi kipya', kukubaliwa na sehemu kubwa ya Watanzania.Jay vilevile ni moja kati ya waanzilishi au wasanii wa awali kabisa katika muziki wa hip hop ya Tanzania.

== Maisha ya muziki ==
Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo [[miaka ya 1990]] na alijiunga na kundi la '[[Hard Blasters Crew]]' (HBC) mwaka [[1994]]. Mwaka [[1995]] Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini [[Tanzania]]. 

Jay na HBC walitoa [[albamu]] ya kwanza iitwayo 'Funaga Kazi' mwaka [[2000]]. Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini [[Tanzania]]. Albamu hii yenye [[ujumbe]] mzito ina nyimbo kama 'Chemsha Bongo' na 'Mamsapu' ambazo zilichangia kufanya muziki wa 'Bongo Flava' kuwa wa kila [[rika]] na kupewa [[heshima]]. Kabla ya hapo muziki huo ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni.

== Msanii binafsi ==
Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo [[2001]] na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo "Machozi Jasho na Damu". Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya apate [[tuzo]] ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa wimbo wake wa 'Ndio Mzee' kutoka kwenye albamu hiyo, wkifuatiwa na wimbo wa "Piga Makofi na  Bongo [[Dar es Salaam]]"

[[Mwaka]] [[2003]] alitoa albamu ya pili iitwayo "Mapinduzi Halisi" ambayo nayo ilishinda tuzo ya [[Kili Music Awards]] kuwa albamu bora ya muziki wa Hip Hop nchini [[Tanzania]] kwa [[mwaka]] [[2003]]. Albamu hii imebeba nyimbo kama "Zali la Mentali", "Msinitenge," na "Promota Anabeep"

[[Mwaka]] [[2006]] [[Januari]] alitoa albamu ya tatu iliyoitwa "J.O.S.E.P.H".  Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka [[Mwanzo]] kabla ya albamu kutoka. Wimbo huu ulichaguliwa kuwa wimbo bora wa [[Bongo Flava]] kwenye [[BBC]] na [[Radio One Awards]].

Mpya imewahi kuteuliwa kuwa albamu bora ya Hip Hop, [[mtunzi]] bora wa nyimbo za Hip Hop, na [[Nyimbo]] bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. [[2006]]."Nikusaidieje" na baadaye [[Kisima Music Awards]] ya [[Kenya]] ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini [[Tanzania]].

== Tuzo Alizopata ==
* '''1''' [[Kili Music Awards]] ([[2003]])
* '''2''' [[BBC]], [[Radio One Awards]] ([[2006]])
* '''3''' [[Kili Music Awards]] ([[2006]])

== Diskografia ==
Hizi ni sehemu ya albamu za muziki alizotoa Nigga Jay

*[[Machozi Jasho na Damu]] (2001)
*[[Mapinduzi Halisi]] (2003)
*[[J.O.S.E.P.H.]] (2006)
*[[Aluta Continua]] (2007)

== Alioshirikiana nao kimuziki ==
* '''1''' [[Lady Jay Dee]]. ( [[Bongo]] [[Dar es Salaam]] na Nimeamini)
* '''2''' [[Mc Babu Ayubu]].   ( Ndio Mzee )
* '''3''' [[Juma Nature]].  ( Ndio Mzee na Zali la Mentali )
* '''4''' [[Q Chilah]].     ( Msinitenge )
* '''5''' [[Inspector Haroun]]. ( Hakuna Noma )
* '''6''' [[Simple X]].          ( Piga Makofi na Hakuna Noma )
* '''7''' [[Jose Chameleone]].    ( Ndivyo Sivyo - Kutoka [[Uganda]] )
* '''8''' [[Adil a.k.a Hisabati]].    ( Tunawakilisha na Rapper Msaidizi kwenye Ziara - Kutoka [[Tanzania]] )

==Tanbihi==
{{reflist}}

==Viungo vya nje==
[http://www.Professorjay.net Professor Jay Tovuti Binafsi]
[http://www.kwetubongo.com Kwetu Bongo]
<p>[http://www.swahiliremix.com Tovuti ya Swahili Remix]</p>

{{Mbegu-wanasiasa-Tanzania}}
[[Jamii:Waliozaliwa 1975]]
[[Jamii:Watu walio hai]]
[[Jamii:Wanasiasa wa Tanzania]]
[[Jamii:Bunge la Tanzania]]
[[Jamii:Wanamuziki wa Tanzania]]