Difference between revisions 910643 and 912175 on swwiki

[[Picha:Sanfranciscoearthquake1906.jpg|thumb|350px|Mji wa [[San Francisco]] ([[Marekani]]) baada ya tetetemo la ardhi la mwaka [[1906]].]]


'''Tetemeko la ardhi'''(zilizala) ni mishtuko ya ghafla ya ardhi. Inatokea mara kwa mara lakini idadi kubwa ni hafifu mno haisikiki na wanadamu ila tu inapimwa na mitambo ya wataalamu.

== Hatari za mitetemeko ya ardhi ==
Tetemeko kubwa laweza kusababisha uharibifu mkubwa na vifo hasa kutokana na majengo yanayoanguka. Baharini tetemeko laweza kusababisha [[tsunami]].

== Sababu ==

Sababu ya tetemeko ni mara nyingi miendo ya [[gandunia]] kama kusukumana kwa [[Bamba la gandunia|mabamba]] ya [[ganda la dunia]]. 
Ili kufahamu sababu hiyo ya matetemeko ya ardhi, inabidi kufahamu mambo yanayoendelea chini ya ardhi.  Kwanza ni lazima kufikiria xd :Wmuundo wa [[dunia]].  Dunia ina umbo la duara.  Umbali uliopo baina ya pande mbili tofauti kinyume za dunia ni kilomita elfu kumi na tatu. Katika sehemu ya nje ya dunia, ardhi ni thabiti (ngumu).  Dunia ina gamba la mwamba ngumu ambalo, kulingana na ukubwa wa dunia yenyewe, ni jembamba. Gamba hilo lina unene ya baina kilomita kumi na kilomita hamsini.

Kama ungeweza kusafiri chini ya ardhi, yaani kuvuka gamba hilo, ungeona kwamba mazingira ni tofauti sana.  Kila kitu kwenye dunia kinavutwa kuelekea sehemu ya kati ya dunia ([[graviti]]).  Kwa hiyo kuna shinikizo kubwa mno chini ya gamba kutokana na 
msukumo kwa vitu vya juu kuelekea chini.  Yote ni mwamba na chuma, lakini kutokana na
shinikizo hilo, kuna joto kali sana, na mwamba na chuma chini ya gamba si imara.  Kwa hiyo mwamba wa chuma umeyeyuka, kama [[lava|matope joto]] yanayotoka nje ya 
volkeno wakati wa [[Mlipuko wa volkeno|mlipuko]].  Ambapo matope hayo yanapokuwa baridi, yanakuwa imara kama 
mwamba wa kawaida. [[magma|Mwamba huo ulioyeyuka wenye joto mno]] unasogea 
ukizunguka chini ya gamba.  Kwa upande wake, gamba linavutwa pia na mwamba ulioyeyuka, likisogea 
pia.  Kwa sababu ya kusukumwa, gamba huvunjika. Kwa hiyo badala ya pande moja zima la gamba, 
kuna baadhi ya [[Bamba la gandunia|mapande makubwa ya gamba]] yanayosogea yakiwa na nguvu kubwa mno.

[[Picha:Quake_epicenters_1963-98_notitle.png‎|right|370px|thumb|Ramani inayoonyesha mahali duniani ambapo nishati ya matetemeko ya ardhi iliachiwa baina ya miaka 1963 na 1998. Kila nukta inaonyesha kitovu cha tetemeko moja.]]

Katika baadhi ya sehemu za dunia, mapande hayo yanakutana yakipambana.  Wakati huo, nguvu kubwa mno 
inasukuma mwamba thabiti wa gamba kuelekea juu na chini.  Ndivyo hivyo baada ya miaka 
mingi sana, safu za milima zinavyojengwa.   Pia pande moja linaposukumwa chini ya pande 
jingine, bonde kubwa sana linajengwa.  Kwa mfano, kuna ufa mkubwa sana uliopo chini ya 
bahari, katika pwani ya [[California|Kalifornia]] magharibi mwa Marekani.  Karibu na pwani ya nchi zilizopo 
katika pwani ya magharibi ya bara la [[Amerika]], kuna milima mingi kutokana na pande hilo 
kusukumwa juu.  Pia, karibu na pwani, kuna mifereji ambapo chini ya bahari imekwenda chini sana, kwa ajili ya 
pande jingine lililosukumwa chini. 

Katika maeneo ambayo mapande yanatenganishwa, gamba ni jembamba, na mwamba ulioyeyuka 
unaondoka.  Ukiona ramani ya dunia, sehemu ya mashariki ya bara la [[Amerika]] na sehemu 
ya magharibi ya mabara ya [[Afrika]] na [[Ulaya]], utaona kwamba inawezekana zamani sana mabara 
hayo yalikuwa bara moja tu.  Pia, katika chini ya bahari kati ya Afrika na Marekani, 
wachunguzi wameona kwamba katika mstari wa katikati baina ya mabara hayo, kuna idadi 
kubwa ya miamba ilioyeyuka iliyotoka ardhini.

Baadhi ya wakati mapande hayo yanateleza pole pole.  Lakini mara kwa 
mara yanasimama badala ya kuendelea kuteleza.  Hivyo nishati inajengeka.  Nishati 
inapoachiwa -- kwa kawaida kwenye mipaka baina ya mapande tofauti -- mapande yanasogea kwa ghafula na kwa haraka.  Hivyo, ardhi inatetemeka. Ndivyo matetemeko ya ardhi yanavyotokea.    Wachunguzi wameona kwamba matetemeko ya ardhi 
mara nyingi yanatokea katika  maeneo hayo ambayo yana milima mingi na nyufa.   Kwa mfano, 
kuna hatari ya matetemeko [[Kalifornia]] nchini [[Marekani]]. 
Mitetemeko mingi yaani zaidi ya asilimia 80 hutokea katika beseni ya [[Pasifiki]].

Katika mazingira ya [[volkeno]] tetemeko lasababishwa na miendo ya [[magma]] chini ya volkeno hasa wakati wa [[Mlipuko wa volkeno|mlipuko]].

== Vipimo ==
Wataalamu hupima tetemeko kwa njia mbalimbali. Kuna skeli mbili zinazotumiwa mara nyingi ni zile za Richter na Mercalli.

<center>
{| class="prettytable" 
|-----
! bgcolor="#cccccc" valign="middle" colspan="6" |
Skeli ya matetemeko ya ardhi kufuatana na Richter na Mercalli 
|----
! bgcolor="#dddddd" rowspan="2" |
Skeli ya [[Charles Francis Richter|Richter]]
! bgcolor="#dddddd" rowspan="2" |
Skeli ya [[Giuseppe Mercalli|Mercalli]]
! bgcolor="#dddddd" rowspan="2" |
Athira
! bgcolor="#dddddd" colspan="2" |
[[nishati]]
! bgcolor="#dddddd" rowspan="2" |
Idadi ya mitetemeko ya ardhi
|-----
! bgcolor="#e0e0e0" |
Tani [[TNT]]
! bgcolor="#e0e0e0" |
[[Joule]]
|-----
| align="center" |
0 hadi 1.9
| align="center" |
I
|
hupimika kwa mitambo tu, haisikiki na wanadamu
|
0.001–0.7
|
(4..4000)<math>\cdot</math>10<sup>6</sup>
| align="center" |
nyingi sana zaidi ya 700,000
|-----
| align="center" |
2 hadi 2.9
| align="center" |
II
|
inasikiwa na watu wachache wakilala 
pinduli huwa na mwendo kidogo
|
1–22
|
(4..90)<math>\cdot</math>10<sup>9</sup>
| align="center" |
300,000
|-----
| align="center" |
3 hadi 3.9
| align="center" |
III
|
husikiwa na watu wachache
mishtuko hulingana na lori linalopita
bilauri zinazokaa pamoja kabatini zinatoa sauti hafifu
|
30–700
|
(0,1..3)<math>\cdot</math>10<sup>12</sup>
| align="center" |
49,000
|-----
| align="center" |
4 hadi 4.9
| align="center" |
IV hadi V
|
hisikiwa na watu wengi. 
Mwendo wa penduli unaonekana kabisa
Bilauri na sahani zatitima, magari huanza kubembea
Vitu vinaweza kuanguka
|
(1–22)<math>\cdot</math>10 
|
(4..90)<math>\cdot</math>10<sup>12</sup>
| align="center" |
6,200
|-----
| align="center" |
5 hadi 5.9
| align="center" |
VI
|
watu hustuka na kukimbia kutoka nyumba zao
viti, kabati na vitanda husukumwa
kuta za nyumba zapata ufa
|
(30–700)<math>\cdot</math>10
|
(0,1..3)<math>\cdot</math>10<sup>15</sup>
| align="center" |
800
|-----
| align="center" |
6 hadi 6.9
| align="center" |
VII hadi IX
|
husikiwa na watu wote wa eneo kwa hofu hata wakiwa kwenye gari
nyumba zaanza kubomolewa
Miti inabembea kama wakati wa upepo mkubwa
Watu hujeruhiwa
Kwenye pwani kuna uwezekano wa mawimbi makubwa (chanzo cha tsunami)
|
(1–22)<math>\cdot</math>10<sup>6</sup> <br /> <small>(kama [[bomu ya nyuklia]] kubwa)</small>
|
(4..90)<math>\cdot</math>10<sup>15</sup>
| align="center" |
120
|-----
| align="center" |
7 hadi 7.9
| align="center" |
X hadi XI
|
watu honesha hofu kubwa wakijaribu kutoka nje ya nyumba kwa namna yoyote; 
nyumba nyingi zaharibiwa ;
ufa zatokea katika ardhi;
mabomba ya maji na gesi yavunjika
watu hujeruhiwa na kuuawa
kwenye pwani tsunami inaweza kutokea
|
(30–700)<math>\cdot</math>10<sup>6</sup><br /> <small>(kama mshtuko wa [[Meteoriti]] ya 100–200 m)</small>
|
(0,1..3)<math>\cdot</math>10<sup>18</sup>
| align="center" |
18
|-----
| align="center" |
8 hadi 8.9
| align="center" |
XII
|
uharibifu mkubwa; majengo yote yanaanguka au hayafai tena; maeneo makubwa yaharibiwa
Kwenye pwani tsunami hadi kina cha mita 40
|
(1–22)<math>\cdot</math>10<sup>9</sup>  
|
(4..90)<math>\cdot</math>10<sup>18</sup>
| align="center" |
kila baada ya miaka 5 
|-----
| align="center" |
9.0 na zaidi 
| align="center" |
—
|
Maafa makubwa; uharibifu kama juu; maisha yote yaweza kuzimwa kimahali

Inawezekana pia: vipande vya uso wa ardhi huhamishwa; visiwa kupotea au kutokea; mabamba ya ganda la dunia yaonekana yamesukumwa;
|
—
|
—
| align="center" |
hakuna tákwimu; tetemeko la aina hili labda kila baada ya miaka 10 hadi 100 
|}
</center>



== Viungo vya Nje ==
* http://earthquake.usgs.gov/activity/past.html

[[Jamii:Gandunia]]
[[Jamii:Maafa asilia]]

{{Link FA|bs}}
{{Link FA|sk}}
{{Link FA|tt}}

[[wa:Tronnmint d' tere]]