Difference between revisions 912175 and 943558 on swwiki

[[Picha:Sanfranciscoearthquake1906.jpg|thumb|350px|Mji wa [[San Francisco]] ([[Marekani]]) baada ya tetetemo la ardhi la mwaka [[1906]].]]


'''Tetemeko la ardhi  '''(pia: '''zilizala''') ni mishtuko ya ghafla ya ardhi. Inatokea mara kwa mara lakini idadi kubwamara nyingi ni hafifu mno haisikiki na wanadamu ila tu inapimwa na mitambo ya wataalamu.

== Hatari za mitetemeko ya ardhi ==
Tetemeko kubwa laweza kusababisha uharibifu mkubwa na vifo hasa kutokana na majengo yanayoanguka. Baharini tetemeko laweza kusababisha [[tsunami]] yaani wimbi kubwa lenye hatari pale linapofika pwani..

== Sababu ==

Sababu ya tetemeko ni mara nyingi miendo ya [[gandunia]] kama kusukumana kwa [[Bamba la gandunia|mabamba]] ya [[ganda la dunia]]. vipande vinavyofanya sehemu ya nje ya dunia. Umbo la dunia unafanana kiasi na chungwa: nje kuna ganda imara (linaitwa [[ganda la dunia]]) na ndani yake sehemu kubwa ni giligili ya moto. Lile ganda la nje si kipande kimoja lakini vipande mbalimbali vinavyoelea juu ya giligili moto ndani ya dunia. Vipande hivi kwa lugha ya kitaalamu huweza kuitwa [[mabamba]] ya [[ganda la dunia]].  Pale ambako vipande hivi vinagusana na kusukumana kunatokea [[msuguano]] na kushikana au kuachana kwa mabamba haya kunasababisha mishtuko ya tetemeko la ardhi. 

Ili kufahamu sababu hiyo ya matetemeko ya ardhi, inabidi kufahamu mambo yanayoendelea chini ya ardhi.  Kwanza ni lazima kufikiria xd :Wmuundo wa [[dunia]].  Dunia ina umbo la duara.  Umbali uliopo baina ya pande mbili tofauti kinyume za dunia ni kilomita elfu kumi na tatu. Katika sehemu ya nje ya dunia, ardhi ni thabiti (ngumu).  Dunia ina gamba la mwamba ngumu ambalo, kulingana na ukubwa wa dunia yenyewe, ni jembamba. Gamba hilo lina unene ya baina kilomita kumi na kilomita hamsini.

(contracted; show full)* http://earthquake.usgs.gov/activity/past.html

[[Jamii:Gandunia]]
[[Jamii:Maafa asilia]]

{{Link FA|bs}}
{{Link FA|sk}}
{{Link FA|tt}}