Difference between revisions 974843 and 976926 on swwiki

'''Zaha''' (pia: '''lava'''; [[ing.]] [[w:lava|lava]]) ni mwamba katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa [[dunia]] mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "[[magma]]" badala ya zaha. 

Zaha inatoka nje kwa kawaida penye [[volkeno]] wakati wa mlipuko. Ikipoa inakuwa [[mwamba]] imara.

Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600[[°C]] hadi 1200 °C. Katika hali hii inasambaa nje ya shimo la [[kasoko]]. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.


<gallery>
Image:Stromboli Eruption.jpg|Mlipuko wa volkeno ya [[Stromboli]] ([[Italia]])- kile chekundu kwenye picha ni zaha.
Image:Aa_large.jpg|Mto wa zaha kwenye volkeno ya [[Kilauea]] ([[Hawaii]])
Image:PahoehoeLava.jpg|Zaha ikipoa inaweza kuonekana hivyo. 
Image:Nyiragongo lava lake.jpg|Ziwa la zaha ndani ya [[kasoko]] ya mlima [[Nyiragongo]] huko [[Goma]] (Kongo)
Image:Kalapana_house_destroyed_by_lava.jpg|Mto wa zaha inavyoharibu nyumba huko Hawaii mwaka 1990
</gallery>

[[Jamii:Volkeno]]
[[Jamii:Jiolojia]]